Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Esta 10:3 - Swahili Revised Union Version

3 Kwa maana Mordekai Myahudi akiwa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwajali watu wake, na kuiangalia hali njema ya wazawa wao wote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Mordekai, Myahudi, alikuwa wa kwanza chini ya mfalme Ahasuero katika madaraka. Alipendwa na kuheshimiwa na Wayahudi, maana aliwafanyia mema watu wake na kuwatakia amani wazawa wao wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Mordekai, Myahudi, alikuwa wa kwanza chini ya mfalme Ahasuero katika madaraka. Alipendwa na kuheshimiwa na Wayahudi, maana aliwafanyia mema watu wake na kuwatakia amani wazawa wao wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Mordekai, Myahudi, alikuwa wa kwanza chini ya mfalme Ahasuero katika madaraka. Alipendwa na kuheshimiwa na Wayahudi, maana aliwafanyia mema watu wake na kuwatakia amani wazawa wao wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Mordekai Myahudi alikuwa wa pili kwa cheo baada ya Mfalme Ahasuero, naye alikuwa bora kabisa na mkuu miongoni mwa Wayahudi. Aliheshimiwa sana na Wayahudi wenzake wengi, kwa sababu alifanya kazi kwa manufaa ya watu wake na kutetea ustawi wa Wayahudi wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Mordekai Myahudi alikuwa wa pili kwa cheo kutoka Mfalme Ahasuero, naye alikuwa bora kabisa miongoni mwa Wayahudi, akipandishwa katika heshima ya juu na ndugu zake Wayahudi kwa sababu aliwatendea mema watu wake, na alizungumza kwa ajili ya ustawi wa Wayahudi wote.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

3 Kwani Myuda Mordekai alikuwa wa pili kwake mfalme Ahaswerosi na mkuu kwa Wayuda, akapendwa na ndugu zake waliokuwa wengi, kwa kuwa aliwatakia mema walio ukoo wake, akasema nao wote walio wa kizazi chake maneno ya utengemano.

Tazama sura Nakili




Esta 10:3
17 Marejeleo ya Msalaba  

Basi wewe utakuwa msimamizi wa nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.


Nawe utakaa katika nchi ya Gosheni, utakuwa karibu nami, wewe, na wanao, na wana wa wanao, na wanyama wako, ng'ombe wako, na yote uliyo nayo. Nami nitakulisha huko;


maana bado imesalia miaka mitano ya njaa; usije ukaingia katika uhitaji, wewe, na nyumba yako, na yote uliyo nayo.


Naye Zikri, mtu hodari wa Efraimu, akawaua Maaseya mwana wa mfalme, na Azrikamu mkuu wa nyumba, na Elkana, aliyekuwa wa pili wake mfalme.


Hata Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, waliposikia habari hizi, ziliwahuzunisha sana, kwa kuwa amekuja mtu kuwatakia heri wana wa Israeli.


Basi palikuwa na Myahudi mmoja huko Susa, mji mkuu; jina lake Mordekai, mwana wa Yairi, mwana wa Shimei, mwana wa Kishi, wa kabila la Benyamini;


Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi langoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo mfalme alivyoamuru wamfanyie. Lakini Mordekai hakumwinamia, wala kumsujudia.


Lakini nimesikia habari zako, kwamba waweza kuleta tafsiri, na kufumbua mafumbo; haya! Kama ukiweza kulisoma andiko hili, na kunijulisha tafsiri yake, utavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utakuwa mtu wa tatu katika ufalme.


Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme.


Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na watawala, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.


Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.


Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu.


Lakini Israeli wote na Yuda wakampenda Daudi; kwa kuwa aliwaongoza wakienda na kurudi vitani.


Akamwambia, Usiogope, kwa maana mkono wa Sauli, babangu, hautakupata; na wewe utakuwa mfalme juu ya Israeli; na mimi nitakuwa makamu wako; ndivyo ajuavyo hata Sauli, babangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo