Methali 21:3 - Swahili Revised Union Version Kutenda haki na hukumu Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kutenda mambo mema na ya haki, humpendeza Mwenyezi-Mungu kuliko tambiko. Biblia Habari Njema - BHND Kutenda mambo mema na ya haki, humpendeza Mwenyezi-Mungu kuliko tambiko. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kutenda mambo mema na ya haki, humpendeza Mwenyezi-Mungu kuliko tambiko. Neno: Bibilia Takatifu Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko dhabihu. Neno: Maandiko Matakatifu Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika zaidi kwa bwana kuliko dhabihu. BIBLIA KISWAHILI Kutenda haki na hukumu Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka. |
BWANA wa majeshi amesema hivi, ya kwamba, Fanyeni hukumu za kweli, kila mtu na amwonee ndugu yake rehema na huruma;
na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhabihu zote pia.
Naye Samweli akasema, Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikiza ushauri kuliko mafuta ya beberu.