Methali 21:15 - Swahili Revised Union Version Ni furaha yao wenye haki kutenda hukumu; Lakini ni uharibifu kwao watendao maovu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Haki ikitekelezwa watu wema hufurahi, lakini watu waovu hufadhaishwa. Biblia Habari Njema - BHND Haki ikitekelezwa watu wema hufurahi, lakini watu waovu hufadhaishwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Haki ikitekelezwa watu wema hufurahi, lakini watu waovu hufadhaishwa. Neno: Bibilia Takatifu Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki, bali hofu kwa watenda maovu. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki, bali kitisho kwa watenda mabaya. BIBLIA KISWAHILI Ni furaha yao wenye haki kutenda hukumu; Lakini ni uharibifu kwao watendao maovu. |
Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
Mimi najua ya kwamba hakuna jema kwao kupita kufurahi, na kufanya mema maadamu wanaishi.
Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?
Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenituma, nikaimalize kazi yake.