Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 64:5 - Swahili Revised Union Version

5 Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Wewe waja kuwasaidia watendao haki kwa furaha, wanaokukumbuka na kuzingatia njia zako. Ulitukasirikia tulipokuwa wenye dhambi; sisi tumeasi kwa muda mrefu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Wewe waja kuwasaidia watendao haki kwa furaha, wanaokukumbuka na kuzingatia njia zako. Ulitukasirikia tulipokuwa wenye dhambi; sisi tumeasi kwa muda mrefu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Wewe waja kuwasaidia watendao haki kwa furaha, wanaokukumbuka na kuzingatia njia zako. Ulitukasirikia tulipokuwa wenye dhambi; sisi tumeasi kwa muda mrefu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Uliwasaidia watu wale watendao yaliyo haki kwa furaha, wale wazikumbukao njia zako. Lakini wakati tulipoendelea kutenda dhambi kinyume na njia zako, ulikasirika. Tutawezaje basi kuokolewa?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Uliwasaidia watu wale watendao yaliyo haki kwa furaha, wale wazikumbukao njia zako. Lakini wakati tulipoendelea kutenda dhambi kinyume na njia zako, ulikasirika. Tutawezaje basi kuokolewa?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?

Tazama sura Nakili

Isaya 64:5
27 Marejeleo ya Msalaba  

Bali fadhili za BWANA ni kwa wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ni kwa vizazi vyote;

Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake.

Njia zote za BWANA ni fadhili na kweli, Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.

Nawe ujifurahishe katika BWANA, Naye atakutimizia haja za moyo wako.

Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo wako, na ng'ombe wako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.

Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.

Nawe utaitia mbele ya lile pazia lililo karibu na sanduku la ushuhuda mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, hapo nitakapokutana nawe.

Maana mtakuwa kama mwaloni ambao majani yake yakauka, na kama bustani isiyo na maji.

Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.

Ee BWANA, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.

Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki.

Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.

Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.

tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako;

Niwezeje kukuacha, Efraimu? Niwezeje kukuachilia Israeli? Niwezeje kukufanya kama Adma? Niwezeje kukuweka kama Seboimu? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja.

Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.

Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika.

Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.

bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.

Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo