Tena Bwana atajiinulia mfalme wa Israeli atakayeiharibu nyumba ya Yeroboamu siku ile; na nini tena hata sasa?
Methali 2:22 - Swahili Revised Union Version Bali waovu watatengwa na nchi, Nao wafanyao hila watang'olewa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini waovu wataondolewa nchini, na wenye hila watangolewa humo. Biblia Habari Njema - BHND Lakini waovu wataondolewa nchini, na wenye hila watangolewa humo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini waovu wataondolewa nchini, na wenye hila watang'olewa humo. Neno: Bibilia Takatifu Bali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi, nao wasio waaminifu watang’olewa kutoka humo. Neno: Maandiko Matakatifu Bali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi, nao wasio waaminifu watang’olewa kutoka humo. BIBLIA KISWAHILI Bali waovu watatengwa na nchi, Nao wafanyao hila watang'olewa. |
Tena Bwana atajiinulia mfalme wa Israeli atakayeiharibu nyumba ya Yeroboamu siku ile; na nini tena hata sasa?
Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa BWANA, kwa sababu ya neno la BWANA, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake,
Wenye dhambi waangamizwe katika nchi, Watendao ubaya wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.
Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao BWANA watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.
Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa.
Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.
Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kufanya mali kimbilio lake.
BWANA hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya BWANA na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na BWANA atalifuta jina lake chini ya mbingu.
BWANA akawang'oa katika nchi yao kwa hasira, na ghadhabu, na makamio makuu, akawatupa waende nchi nyingine, kama hivi leo.
Naye BWANA, Mungu wako, atayatupilia mbali mataifa yale mbele yako kidogo kidogo; haikupasi kuwaangamiza kwa mara moja, wasije wakaongezeka kwako wanyama wa mwitu.