Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile mkononi mwake.
Methali 19:27 - Swahili Revised Union Version Mwanangu, acha kusikia mafundisho, Ukitaka tu kuyaasi maneno ya maarifa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho, utapotea mara mbali na maneno ya hekima. Biblia Habari Njema - BHND Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho, utapotea mara mbali na maneno ya hekima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho, utapotea mara mbali na maneno ya hekima. Neno: Bibilia Takatifu Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho, utatangatanga mbali na maneno ya maarifa. Neno: Maandiko Matakatifu Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho, utatangatanga mbali na maneno ya maarifa. BIBLIA KISWAHILI Mwanangu, acha kusikia mafundisho, Ukitaka tu kuyaasi maneno ya maarifa. |
Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile mkononi mwake.
Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliosema nawe, wakinena, Baba yako alilifanya kongwa letu kuwa zito, lakini wewe tufanyie jepesi; uwaambie hivi, Kidole changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.
Lakini, kuhusu habari zenu, msisikilize manabii wenu, wala wabashiri wenu, wala ndoto zenu, wala watambuzi wenu, wala waganga wenu, wanaowaambia, ya kwamba, Hamtamtumikia mfalme wa Babeli;
Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali.
Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.
ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zipimeni hizo roho, kama zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.
Ninayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wanaojiita mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;