Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Methali 15:3 - Swahili Revised Union Version Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Macho ya Mwenyezi-Mungu huona kila kitu, humchunguza mtu mwema na mtu mbaya. Biblia Habari Njema - BHND Macho ya Mwenyezi-Mungu huona kila kitu, humchunguza mtu mwema na mtu mbaya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Macho ya Mwenyezi-Mungu huona kila kitu, humchunguza mtu mwema na mtu mbaya. Neno: Bibilia Takatifu Macho ya Mwenyezi Mungu yako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema. Neno: Maandiko Matakatifu Macho ya bwana yako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema. BIBLIA KISWAHILI Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema. |
Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari.
Maana macho yangu yaziangalia njia zao zote, hawakufichwa uso wangu usiwaone, wala haukusitirika uovu wao macho yangu yasiuone.
Je, mtu yeyote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.
mkuu wa mashauri, muweza katika kutenda; ambaye macho yake yamefumbuka juu ya njia zote za wanadamu, kumpa kila mtu kwa kadiri ya njia zake, na kwa kadiri ya matunda ya matendo yake,
Maana yeyote aliyeidharau siku ya mambo madogo watafurahi, naye ataiona timazi ikiwa katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi taa saba ndizo macho ya BWANA; yanaona huku na huko duniani kote.
Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.