Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zekaria 4:10 - Swahili Revised Union Version

10 Maana yeyote aliyeidharau siku ya mambo madogo watafurahi, naye ataiona timazi ikiwa katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi taa saba ndizo macho ya BWANA; yanaona huku na huko duniani kote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Maendeleo ya ujenzi wa hekalu yanaonekana madogo, na watu wanayadharau; lakini watamwona Zerubabeli akiendelea kulijenga hekalu, nao watafurahi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Maendeleo ya ujenzi wa hekalu yanaonekana madogo, na watu wanayadharau; lakini watamwona Zerubabeli akiendelea kulijenga hekalu, nao watafurahi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Maendeleo ya ujenzi wa hekalu yanaonekana madogo, na watu wanayadharau; lakini watamwona Zerubabeli akiendelea kulijenga hekalu, nao watafurahi.” Huyo malaika akaniambia, “Hizo taa saba ni macho saba ya Mwenyezi-Mungu yaonayo kila mahali duniani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 “Ni nani atakayeidharau siku ya mambo madogo? Macho saba ya Mwenyezi Mungu, yanayozunguka dunia yote, yatashangilia yatakapoona jiwe la juu kabisa likiwa mkononi mwa Zerubabeli!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 “Ni nani anayeidharau siku ya mambo madogo? Watu watashangilia watakapoona timazi mkononi mwa Zerubabeli. “(Hizi saba ni macho ya bwana ambayo huzunguka duniani kote.)”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Maana yeyote aliyeidharau siku ya mambo madogo watafurahi, naye ataiona timazi ikiwa katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi taa saba ndizo macho ya BWANA; yanaona huku na huko duniani kote.

Tazama sura Nakili




Zekaria 4:10
26 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.


Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.


Akiwa katika kiti chake cha enzi. Huwaangalia wote wakaao duniani.


Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.


Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing'aayo, Ikizidi kung'aa hata mchana mkamilifu.


mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake.


Nanyi mtaona, na mioyo yenu itafurahi, na mifupa yenu itasitawi kama majani mabichi; na mkono wa BWANA utajulikana, uwaelekeao watumishi wake, naye atawaonea adui zake ghadhabu.


Maana macho yangu yaziangalia njia zao zote, hawakufichwa uso wangu usiwaone, wala haukusitirika uovu wao macho yangu yasiuone.


Na wale viumbe hai walipiga mbio, kwenda na kurudi, kama kuonekana kwa kumulika kwa umeme.


Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.


Ikawa, nzige walipokwisha kula majani ya nchi, ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, samehe, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo.


Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, acha, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo.


Miongoni mwenu amebaki nani aliyeiona nyumba hii katika utukufu wake wa kwanza? Nanyi mnaionaje sasa? Je! Mbele ya macho yenu, siyo kama si kitu?


Maana, litazame jiwe hili nililoliweka mbele ya Yoshua; katika jiwe moja ziko nyuso saba; tazama, nitachonga maandishi yake, asema BWANA wa majeshi, nami nitauondoa uovu wa nchi hii katika siku moja.


Ufunuo wa neno la BWANA, lililosemwa juu ya nchi ya Hadraki, na Dameski itakuwa mahali pake pa kustarehe; kwa maana jicho la mwanadamu na la kabila zote za Israeli linamwelekea BWANA;


Bali ilibidi kusherehekea na kushangilia kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.


Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.


Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo