Methali 15:29 - Swahili Revised Union Version BWANA yuko mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu yuko mbali na watu waovu, lakini yu karibu na watu wema kuwasikiliza. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu yuko mbali na watu waovu, lakini yu karibu na watu wema kuwasikiliza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu yuko mbali na watu waovu, lakini yu karibu na watu wema kuwasikiliza. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu yuko mbali na waovu, bali husikia maombi ya wenye haki. Neno: Maandiko Matakatifu bwana yuko mbali na waovu, bali husikia maombi ya wenye haki. BIBLIA KISWAHILI BWANA yuko mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki. |
lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Tunajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.
Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana uko juu ya watenda mabaya.