Methali 14:12 - Swahili Revised Union Version Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Njia unayodhani kuwa ni sawa, mwishoni yaweza kukuongoza kwenye kifo. Biblia Habari Njema - BHND Njia unayodhani kuwa ni sawa, mwishoni yaweza kukuongoza kwenye kifo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Njia unayodhani kuwa ni sawa, mwishoni yaweza kukuongoza kwenye kifo. Neno: Bibilia Takatifu Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini. Neno: Maandiko Matakatifu Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini. BIBLIA KISWAHILI Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti. |
Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akatengeneza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri.
Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.
Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti.
Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.