Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 14:13 - Swahili Revised Union Version

13 Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Huzuni yaweza kufichika katika kicheko; baada ya furaha huja majonzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Huzuni yaweza kufichika katika kicheko; baada ya furaha huja majonzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Huzuni yaweza kufichika katika kicheko; baada ya furaha huja majonzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Hata katika kicheko moyo unaweza kuuma, nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Hata katika kicheko moyo waweza kuuma, nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo.

Tazama sura Nakili




Methali 14:13
9 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili.


Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.


Nikauambia moyo wangu, Haya, nitakujaribu kwa njia ya furaha basi ujifurahishe kwa anasa. Na tazama, hayo nayo yakawa ubatili.


Nikasema juu ya kicheko, Ni wazimu; na juu ya furaha, Yafaa nini?


Abrahamu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo yako mema katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unateseka.


Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni kubwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo