Akawachukua mateka watu wa Yerusalemu wote pia, na wakuu wote, na mashujaa wote, watu elfu kumi; na mafundi wote, na wafua chuma wote; hapana mtu aliyebaki, ila waliokuwa wanyonge wa watu wa nchi.
Methali 13:8 - Swahili Revised Union Version Fidia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake; Bali mtu maskini hasikii ogofyo lolote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Fidia ya mtu ni mali yake, lakini maskini hana cha kutishwa. Biblia Habari Njema - BHND Fidia ya mtu ni mali yake, lakini maskini hana cha kutishwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Fidia ya mtu ni mali yake, lakini maskini hana cha kutishwa. Neno: Bibilia Takatifu Utajiri wa mtu unaweza kukomboa maisha yake, bali mtu maskini hasikii kitisho. Neno: Maandiko Matakatifu Utajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake, bali mtu maskini hasikii kitisho. BIBLIA KISWAHILI Fidia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake; Bali mtu maskini hasikii ogofyo lolote. |
Akawachukua mateka watu wa Yerusalemu wote pia, na wakuu wote, na mashujaa wote, watu elfu kumi; na mafundi wote, na wafua chuma wote; hapana mtu aliyebaki, ila waliokuwa wanyonge wa watu wa nchi.
Lakini huyo kamanda wa askari walinzi akawaacha watu walio maskini ili wawe watunza mizabibu na wakulima.
Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake.
Lakini akiandikiwa ukombozi, ndipo atakapotoa kwa ajili ya uhai wake hicho atakachoandikiwa.
Kuna mtu anayejitajirisha, lakini hana kitu; Kuna anayejifanya kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.
Lakini Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawaacha baadhi ya maskini wa watu, waliokuwa hawana kitu, katika nchi ya Yuda, akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba wakati uo huo.
Lakini watu kumi walionekana miongoni mwao, waliomwambia Ishmaeli, Usituue; kwa maana tuna akiba zetu zilizofichwa shambani, za ngano, na shayiri, na mafuta, na asali. Basi, akawaacha, asiwaue watu hao pamoja na ndugu zao.
Lakini nitabakiza ndani yako watu walioonewa na maskini, nao watalitumainia jina la BWANA.
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kuipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?