Basi, msiwape wana wao binti zenu, wala msitwae binti zao kuwa wake za wana wenu, wala msiwatakie amani wala kufanikiwa milele; ili mpate kuwa hodari, na kula wema wa nchi hiyo, na kuwaachia watoto wenu iwe urithi wa milele.
Methali 13:22 - Swahili Revised Union Version Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mwema huwaachia urithi uzao wake, lakini mali ya mwenye dhambi imerundikiwa waadilifu. Biblia Habari Njema - BHND Mtu mwema huwaachia urithi uzao wake, lakini mali ya mwenye dhambi imerundikiwa waadilifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mwema huwaachia urithi uzao wake, lakini mali ya mwenye dhambi imerundikiwa waadilifu. Neno: Bibilia Takatifu Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi, bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa kwa ajili ya wenye haki. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi, bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa kwa ajili ya wenye haki. BIBLIA KISWAHILI Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki. |
Basi, msiwape wana wao binti zenu, wala msitwae binti zao kuwa wake za wana wenu, wala msiwatakie amani wala kufanikiwa milele; ili mpate kuwa hodari, na kula wema wa nchi hiyo, na kuwaachia watoto wenu iwe urithi wa milele.
Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzawa wake akiomba chakula.
Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.