Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Methali 13:10 - Swahili Revised Union Version

Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kiburi husababisha tu ugomvi, lakini kwa wanaokubali shauri jema mna hekima.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kiburi husababisha tu ugomvi, lakini kwa wanaokubali shauri jema mna hekima.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kiburi husababisha tu ugomvi, lakini kwa wanaokubali shauri jema mna hekima.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kiburi huzalisha magomvi tu, bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kiburi huzalisha magomvi tu, bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Methali 13:10
23 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! Nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao.


Kweli umepiga Edomu, na moyo wako umekutukuza; ujisifu basi, ukae nyumbani mwako. Mbona unataka kujitia bure katika madhara, hata uanguke, wewe na Yuda pamoja nawe?


Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.


Nuru ya mwenye haki yang'aa sana; Bali taa ya mtu mbaya itazimika.


Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji; Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.


Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho, Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho.


Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana; Na kwa shauri la akili fanya vita.


Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.


Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania; Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye, Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha.


Mwenye nafsi ya kutamani huchochea fitina; Bali amtumainiye BWANA ataneemeshwa.


Yakatokea mashindano kati yao, kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa.


amejivuna; wala hafahamu neno lolote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matusi, na shuku mbaya;


Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?


Basi ikawa, wote waliolishuhudia jambo hilo wakasema, Jambo kama hili halijatendeka wala kuonekana tangu siku hiyo wana wa Israeli walipokwea kutoka katika nchi ya Misri hadi leo; haya, lifikirini, fanyeni shauri, na mliseme.