Afadhali mtu anayedharauliwa, ikiwa ana mtumwa, Kuliko ajisifuye, ikiwa anahitaji chakula.
Methali 12:10 - Swahili Revised Union Version Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mwadilifu huwajali wanyama wake, lakini huruma ya mwovu ni ukatili. Biblia Habari Njema - BHND Mtu mwadilifu huwajali wanyama wake, lakini huruma ya mwovu ni ukatili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mwadilifu huwajali wanyama wake, lakini huruma ya mwovu ni ukatili. Neno: Bibilia Takatifu Mtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake, bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake, bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili. BIBLIA KISWAHILI Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili. |
Afadhali mtu anayedharauliwa, ikiwa ana mtumwa, Kuliko ajisifuye, ikiwa anahitaji chakula.
hata nije nikawachukue mpaka nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu.
Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai?
Kwa maana katika Torati ya Musa imeandikwa, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Je! Hapo Mungu aangalia mambo ya ng'ombe?
Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?
Adoni-bezeki akasema, Wafalme sabini, waliokuwa wamekatwa vidole vyao vya gumba vya mikono na vya miguu, waliokota chakula chao chini ya meza yangu; kama nilivyofanya mimi, Mungu amenilipa vivyo hivyo. Wakamleta Yerusalemu naye akafa kuko.
Huyo Nahashi, Mwamoni, akawaambia, Kwa sharti hili mimi nitapatana nanyi, kila mtu ang'olewe jicho la kulia; na kwa jambo hilo nitawashutumu Waisraeli wote pia.