Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Methali 11:28 - Swahili Revised Union Version Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayetegemea mali zake ataanguka, lakini mwadilifu atastawi kama jani bichi. Biblia Habari Njema - BHND Anayetegemea mali zake ataanguka, lakini mwadilifu atastawi kama jani bichi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayetegemea mali zake ataanguka, lakini mwadilifu atastawi kama jani bichi. Neno: Bibilia Takatifu Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka, bali mwenye haki atastawi kama jani bichi. Neno: Maandiko Matakatifu Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka, bali mwenye haki atastawi kama jani bichi. BIBLIA KISWAHILI Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani. |
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang'anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
Watu wako nao watakuwa wenye haki wote, Nao watairithi nchi milele; Wao ni chipukizi nililolipanda mimi mwenyewe, Kazi ya mikono yangu mwenyewe, Ili mimi nitukuzwe.
Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa joto ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.
Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.