Methali 11:2 - Swahili Revised Union Version Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kiburi huandamana na fedheha, lakini kwa watu wanyenyekevu mna hekima. Biblia Habari Njema - BHND Kiburi huandamana na fedheha, lakini kwa watu wanyenyekevu mna hekima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kiburi huandamana na fedheha, lakini kwa watu wanyenyekevu mna hekima. Neno: Bibilia Takatifu Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima. Neno: Maandiko Matakatifu Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima. BIBLIA KISWAHILI Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. |
Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.
Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; uache dhambi zako kwa kutenda haki, uache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za fanaka.
Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.