Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Methali 11:10 - Swahili Revised Union Version

Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu wanapoangamia, watu hushangilia.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Waadilifu wakipata fanaka mji hushangilia, na waovu wakiangamia watu hupiga vigelegele.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Waadilifu wakipata fanaka mji hushangilia, na waovu wakiangamia watu hupiga vigelegele.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Waadilifu wakipata fanaka mji hushangilia, na waovu wakiangamia watu hupiga vigelegele.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi; mwovu anapoangamia, kuna shangwe za furaha.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi; mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu wanapoangamia, watu hushangilia.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Methali 11:10
14 Marejeleo ya Msalaba  

Basi watu wote wa nchi wakafurahi, na mji ukatulia. Naye Athalia wakamwua kwa upanga karibu na nyumba ya mfalme.


akatazama, na angalia, mfalme amesimama karibu na nguzo yake mlangoni, nao makamanda na wenye parapanda karibu na mfalme; wakafurahi watu wote wa nchi, wakapiga parapanda; waimbaji pia wakipiga vinanda, wakaongoza nyimbo za kusifu. Ndipo Athalia akararua mavazi yake, akasema, Uhaini! Uhaini!


Basi wakafurahi watu wote wa nchi, na mji ukatulia baada ya Athalia kuuawa kwa upanga.


Watu watampigia makofi, Na kumzomea atoke mahali pake.


Miriamu akawaitikia, Mwimbieni BWANA kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.


Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.


Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi; Bali waovu waondokapo, watu hujificha.


Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha; Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.


Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua.


Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjia kutoka kaskazini, asema BWANA.


Na waangamie vivyo hivyo adui zako wote, Ee BWANA. Bali wao wampendao na wawe kama jua hapo litokapo kwa nguvu zake. Nayo nchi ikastarehe miaka arubaini.