Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.
Methali 10:26 - Swahili Revised Union Version Kama siki menoni, na kama moshi machoni, Ndivyo alivyo mtu mvivu kwa hao waliomwajiri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama ilivyo siki kwa meno au moshi machoni, ndivyo alivyo mvivu kwa bwana wake. Biblia Habari Njema - BHND Kama ilivyo siki kwa meno au moshi machoni, ndivyo alivyo mvivu kwa bwana wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama ilivyo siki kwa meno au moshi machoni, ndivyo alivyo mvivu kwa bwana wake. Neno: Bibilia Takatifu Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho, ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma. Neno: Maandiko Matakatifu Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho, ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma. BIBLIA KISWAHILI Kama siki menoni, na kama moshi machoni, Ndivyo alivyo mtu mvivu kwa hao waliomwajiri. |
Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.
Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito, Ni kama yeye avuaye nguo wakati wa baridi; Ni kama siki juu ya magadi.
watu wasemao, Simama peke yako, usinikaribie mimi, kwa maana mimi ni mtakatifu kuliko wewe; watu hao ni moshi puani mwangu, moto uwakao mchana kutwa.
Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;