Methali 10:15 - Swahili Revised Union Version Mali ya tajiri ndio ngome yake; Ufukara wa maskini ndio umwangamizao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mali ya tajiri ndio ngome yake, umaskini wa maskini humletea maangamizi. Biblia Habari Njema - BHND Mali ya tajiri ndio ngome yake, umaskini wa maskini humletea maangamizi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mali ya tajiri ndio ngome yake, umaskini wa maskini humletea maangamizi. Neno: Bibilia Takatifu Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, bali ufukara ni maangamizi ya maskini. Neno: Maandiko Matakatifu Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, bali ufukara ni maangamizi ya maskini. BIBLIA KISWAHILI Mali ya tajiri ndio ngome yake; Ufukara wa maskini ndio umwangamizao. |
Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kufanya mali kimbilio lake.
Ndugu zote wa maskini humchukia; Jinsi gani rafiki zake huzidi kujitenga naye! Huwafuata kwa maneno, lakini wametoweka.
Kwa maana ulinzi wa hekima ni kama ulinzi wa fedha na ubora wa maarifa ni kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.
BWANA asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;
Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.