Methali 10:12 - Swahili Revised Union Version Kuchukiana huleta fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Chuki huzusha ugomvi, lakini upendo hufunika makosa yote. Biblia Habari Njema - BHND Chuki huzusha ugomvi, lakini upendo hufunika makosa yote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Chuki huzusha ugomvi, lakini upendo hufunika makosa yote. Neno: Bibilia Takatifu Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote. Neno: Maandiko Matakatifu Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote. BIBLIA KISWAHILI Kuchukiana huleta fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote. |
Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.
Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?
jueni ya kuwa yeye amrejeshaye mwenye dhambi hadi akatoka katika njia ya upotevu, ataokoa roho ya mwenye dhambi kutoka mauti, na kufunika wingi wa dhambi.
Zaidi ya yote iweni na bidii kubwa katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.