Mathayo 27:18 - Swahili Revised Union Version Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa ajili ya husuda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alisema hivyo maana alijua wazi kwamba walimleta kwake kwa sababu ya wivu. Biblia Habari Njema - BHND Alisema hivyo maana alijua wazi kwamba walimleta kwake kwa sababu ya wivu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alisema hivyo maana alijua wazi kwamba walimleta kwake kwa sababu ya wivu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa alitambua kwamba walikuwa wamemkabidhi Isa kwake kwa ajili ya wivu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa alitambua Isa alikuwa amekabidhiwa kwake kwa ajili ya wivu. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa ajili ya husuda. |
Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.
BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.
Basi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo?
Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.
Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana.
Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), wamejaa wivu,
Au mwadhani ya kwamba Maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?