Basi wakati wa sikukuu, mtawala desturi yake huwafungulia mkutano mfungwa mmoja waliyemtaka.
Mathayo 27:16 - Swahili Revised Union Version Basi palikuwa na mfungwa mashuhuri siku zile, aitwaye Baraba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati huo kulikuwa na mfungwa aliyejulikana sana, jina lake Baraba. Biblia Habari Njema - BHND Wakati huo kulikuwa na mfungwa aliyejulikana sana, jina lake Baraba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati huo kulikuwa na mfungwa aliyejulikana sana, jina lake Baraba. Neno: Bibilia Takatifu Palikuwa na mfungwa mmoja mwenye sifa mbaya, aliyeitwa Baraba. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati huo alikuwepo mfungwa mmoja mwenye sifa mbaya, aliyeitwa Baraba. BIBLIA KISWAHILI Basi palikuwa na mfungwa mashuhuri siku zile, aitwaye Baraba. |
Basi wakati wa sikukuu, mtawala desturi yake huwafungulia mkutano mfungwa mmoja waliyemtaka.
Basi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo?
Palikuwa na mtu aitwaye Baraba, aliyefungwa pamoja na waasi, waliosababisha mauaji katika uhalifu huo.
Akamfungua yule aliyetupwa gerezani kwa ajili ya fitina na uuaji, yule waliyemtaka, akamtoa Yesu wamfanyie watakavyo.
Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang'anyi.
ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.
Nisalimieni Androniko na Yunia, jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, ambao ni maarufu miongoni mwa mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.