Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
Mathayo 26:4 - Swahili Revised Union Version wakafanya shauri pamoja, ili wamkamate Yesu kwa hila na kumwua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue. Biblia Habari Njema - BHND Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue. Neno: Bibilia Takatifu Wakapanga kumkamata Isa kwa siri na kumuua. Neno: Maandiko Matakatifu Wakafanya shauri ili kumkamata Isa kwa siri na kumuua. BIBLIA KISWAHILI wakafanya shauri pamoja, ili wamkamate Yesu kwa hila na kumwua. |
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,
Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;
Baada ya siku mbili ilikuwa sikukuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa; wakuu wa makuhani na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua.
akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyooka?
Huyo akawafanyia hila kabila yetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru wawatupe watoto wao wachanga, ili wasiishi.
Lakini nahofu; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.