Mathayo 23:12 - Swahili Revised Union Version Na yeyote atakayejikweza, atadhiliwa; na yeyote atakayejidhili, atakwezwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa. Biblia Habari Njema - BHND Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa yeyote anayejikweza atashushwa, na yeyote anayejinyenyekeza atakwezwa. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa yeyote anayejikweza atashushwa, na yeyote anayejinyenyekeza atakwezwa. BIBLIA KISWAHILI Na yeyote atakayejikweza, atadhiliwa; na yeyote atakayejidhili, atakwezwa. |
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.
Basi, yeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.