Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 4:37 - Swahili Revised Union Version

37 Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

37 “Na sasa, mimi Nebukadneza ninamsifu na kumtukuza na kumheshimu mfalme wa mbinguni. Maana matendo yake yote ni ya haki, naye huwashusha wenye kiburi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

37 “Na sasa, mimi Nebukadneza ninamsifu na kumtukuza na kumheshimu mfalme wa mbinguni. Maana matendo yake yote ni ya haki, naye huwashusha wenye kiburi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

37 “Na sasa, mimi Nebukadneza ninamsifu na kumtukuza na kumheshimu mfalme wa mbinguni. Maana matendo yake yote ni ya haki, naye huwashusha wenye kiburi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

37 Basi mimi, Nebukadneza, humhimidi, na humtukuza na kumsifu Mfalme wa mbinguni, kwa sababu kila kitu anachofanya ni haki, na njia zake zote ni adili. Nao wanaoenda kwa kiburi anaweza kuwashusha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

37 Basi mimi, Nebukadneza, humhimidi, na humtukuza na kumsifu Mfalme wa mbinguni, kwa sababu kila kitu afanyacho ni haki, na njia zake zote ni adili. Nao waendao kwa kiburi anaweza kuwashusha.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

37 Sasa mimi Nebukadinesari ninamsifu mfalme wa mbinguni na kumkuza na kumtukuza, kwani matendo yake yote ni ya kweli, njia zake ni za wongofu, nao waendeleao kujikuza anaweza kuwanyenyekeza.

Tazama sura Nakili




Danieli 4:37
31 Marejeleo ya Msalaba  

Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia Maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika Kumbukumbu ya Hozai.


Basi mfalme akamwambia Hamani, Hima! Twaa mavazi na farasi kama ulivyosema, ukamfanyie vivyo hivyo Mordekai, Myahudi, aketiye mlangoni pa mfalme; lisipungue neno lolote katika yote uliyoyasema.


Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, Ee BWANA, na kwa uaminifu umenitesa.


Mfalme mkuu upendaye hukumu kwa haki; Umeiimarisha haki; Umefanya hukumu na haki katika Israeli.


Sasa najua ya kuwa BWANA ni mkuu kuliko miungu yote; naam, katika jambo hilo walilowatenda kwa ujeuri.


Kisha hao vyura watakwea juu yako wewe, na juu ya watu wako, na juu ya watumishi wako wote.


BWANA wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia.


bali BWANA wa majeshi ametukuzwa katika hukumu, na Mungu aliye Mtakatifu ametakaswa katika haki.


Waiteni wapiga mishale juu ya Babeli, Naam, wote waupindao upinde; Pangeni hema kumzunguka pande zote; Ili asiokoke hata mtu mmoja wao; Mlipeni kwa kadiri ya kazi yake; Mtendeni sawasawa na yote aliyoyatenda; Kwa sababu amefanya kiburi juu ya BWANA, Juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.


Kwa maana dada yako, Sodoma, hakutajwa kwa kinywa chako katika siku ya kiburi chako;


upate kukumbuka, na kufadhaika, usifumbue kinywa chako tena, kwa sababu ya aibu yako; hapo nitakapokusamehe yote uliyoyatenda, asema Bwana MUNGU.


Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala.


Ishara zake ni kubwa kama nini! Na maajabu yake yana uweza kama nini! Ufalme wake ni ufalme wa milele; na mamlaka yake ni ya kizazi hata kizazi.


Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadneza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;


Wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe.


Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.


Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;


Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.


Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.


Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni za kweli, na haki.


Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa, Naye huyapima matendo kwa mizani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo