Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 5:1 - Swahili Revised Union Version

1 Mfalme Belshaza, aliwafanyia wakuu wake elfu karamu kubwa akanywa divai mbele ya hao elfu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Siku moja mfalme Belshaza aliwaandalia karamu kubwa maelfu ya wakuu wake na kunywa divai pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Siku moja mfalme Belshaza aliwaandalia karamu kubwa maelfu ya wakuu wake na kunywa divai pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Siku moja mfalme Belshaza aliwaandalia karamu kubwa maelfu ya wakuu wake na kunywa divai pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Mfalme Belshaza aliandaa karamu kubwa kwa ajili ya wakuu wake elfu moja, na akanywa mvinyo pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Mfalme Belshaza alifanya karamu kubwa kwa ajili ya maelfu ya wakuu wake na akanywa mvinyo pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

1 Mfalme Belsasari aliwafanyia wakuu wake elfu karamu kubwa, akanywa mvinyo mbele yao hao elfu.

Tazama sura Nakili




Danieli 5:1
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao, akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji, na cha mkuu wa waokaji, miongoni mwa watumwa wake.


mwaka wa tatu wa kutawala kwake, ikawa aliwafanyia karamu wakuu na mawaziri wake; wakuu wa majeshi ya Uajemi na Umedi; watu maarufu na wakuu wa mikoa, wakihudhuria mbele zake.


Siku hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung'oa nywele zao, na kuvaa nguo za magunia;


Na yeye BWANA wa majeshi akafunua haya masikioni mwangu, Ni kweli, uovu huu hautatakaswa wala kuwatokeni hata mfe; asema Bwana, BWANA wa majeshi.


Upanga uko juu ya Wakaldayo, asema BWANA, na juu yao wakaao Babeli, na juu ya wakuu wake, na juu ya watu wake wenye hekima.


Wakiingiwa na ukali, nitawafanyia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema BWANA.


Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, watawala wake, na makamanda wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA.


Usiku huo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, akauawa.


Kwa maana kama miiba wametatana, kama walevi wamelewa, watateketezwa kama mabua makavu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo