Mathayo 22:43 - Swahili Revised Union Version Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akawaambia, “Basi, inawezekanaje kwamba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana? Maana alisema: Biblia Habari Njema - BHND Yesu akawaambia, “Basi, inawezekanaje kwamba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana? Maana alisema: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akawaambia, “Basi, inawezekanaje kwamba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana? Maana alisema: Neno: Bibilia Takatifu Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi, akinena kwa kuongozwa na Roho wa Mungu, anamwita Al-Masihi ‘Bwana’? Kwa maana asema, Neno: Maandiko Matakatifu Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi, akinena kwa kuongozwa na Roho, anamwita Al-Masihi ‘Bwana’? Kwa maana asema, BIBLIA KISWAHILI Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema, |
Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kulia, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Ndugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu;
Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.
Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Nilikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
Na mara nilikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti;