Mathayo 22:33 - Swahili Revised Union Version Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia mafundisho yake. Biblia Habari Njema - BHND Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia mafundisho yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia mafundisho yake. Neno: Bibilia Takatifu Wale umati wa watu waliposikia hayo, walishangaa sana kwa mafundisho yake. Neno: Maandiko Matakatifu Ule umati wa watu uliposikia hayo, ulishangaa sana kwa mafundisho yake. BIBLIA KISWAHILI Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake. |
Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana.
Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?
Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?