Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.
Mathayo 21:39 - Swahili Revised Union Version Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, wakamkamata, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamuua. Biblia Habari Njema - BHND Basi, wakamkamata, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamuua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, wakamkamata, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamuua. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua. BIBLIA KISWAHILI Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. |
Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.
Yesu akamwambia, Rafiki, fanya ulilolijia. Wakaenda, wakanyosha mikono yao wakamkamata Yesu.
Nao waliomkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokuwa wamekutanika waandishi na wazee.
Basi wale askari na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi walimkamata Yesu, wakamfunga.
mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulubisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua;
jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulubisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama akiwa mzima mbele yenu.
Ni yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumwudhi? Nao waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki; ambaye ninyi sasa mmekuwa wasaliti wake, mkamwua;