Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Mathayo 16:6 - Swahili Revised Union Version

Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Yesu akawaambia, “Muwe macho na mjihadhari na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Yesu akawaambia, “Muwe macho na mjihadhari na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Yesu akawaambia, “Muwe macho na mjihadhari na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo!”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Isa akawaambia, “Jihadharini. Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Isa akawaambia, “Jihadharini. Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Mathayo 16:6
15 Marejeleo ya Msalaba  

Sadaka ya unga yoyote itakayosongezwa kwa BWANA isitiwe chachu kabisa; kwa kuwa hamtateketeza chachu, wala asali yoyote, kuwa ni sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.


Wakamjia Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaoneshe ishara itokayo mbinguni.


Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa sikuwaambia kwa sababu ya mkate? Ila jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.


Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.


Nao wanafunzi wakaenda hadi ng'ambo, wakasahau kuchukua mikate.


Wakabishana wao kwa wao, wakisema, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate.


Na alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazawa wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?


Akawaagiza, akasema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode.


Wakati huo, makutano walipokutanika maelfu, hata wakakanyagana, alianza kuwaambia wanafunzi wake kwanza, Jilindeni na chachu ya Mafarisayo, ambayo ni unafiki.


Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.


Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula?


Chachu kidogo huchachua donge zima.