Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Walawi 2:11 - Swahili Revised Union Version

11 Sadaka ya unga yoyote itakayosongezwa kwa BWANA isitiwe chachu kabisa; kwa kuwa hamtateketeza chachu, wala asali yoyote, kuwa ni sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 “Sadaka yoyote ya nafaka utakayomletea Mwenyezi-Mungu ni lazima iwe imetengenezwa bila chachu; kwani hakuna ruhusa kamwe kutumia chachu wala asali katika sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 “Sadaka yoyote ya nafaka utakayomletea Mwenyezi-Mungu ni lazima iwe imetengenezwa bila chachu; kwani hakuna ruhusa kamwe kutumia chachu wala asali katika sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 “Sadaka yoyote ya nafaka utakayomletea Mwenyezi-Mungu ni lazima iwe imetengenezwa bila chachu; kwani hakuna ruhusa kamwe kutumia chachu wala asali katika sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 “ ‘Kila sadaka ya nafaka unayoleta kwa Mwenyezi Mungu ni lazima ifanywe bila kutiwa chachu, kwa kuwa huna ruhusa kuchoma chachu yoyote au asali katika sadaka inayotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 “ ‘Kila sadaka ya nafaka unayoleta kwa bwana ni lazima ifanywe bila kutiwa chachu, kwa kuwa huna ruhusa kuchoma chachu yoyote au asali katika sadaka itolewayo kwa bwana kwa moto.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Sadaka ya unga yoyote itakayosongezwa kwa BWANA isitiwe chachu kabisa; kwa kuwa hamtateketeza chachu, wala asali yoyote, kuwa ni sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.

Tazama sura Nakili

Walawi 2:11
19 Marejeleo ya Msalaba  

Usinitolee damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hadi asubuhi.

Kisha uvitwae vile vitu mikononi mwao, na kuviteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa, viwe harufu nzuri mbele ya BWANA; ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.

Usisongeze damu ya sadaka yangu pamoja na mkate uliotiwa chachu; wala hiyo sadaka ya sikukuu ya Pasaka haitasazwa hata asubuhi.

Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo.

Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha; Usije ukashiba na kuitapika.

Haifai kula asali nyingi mno; Vile vile mtu kutafuta utukufu wake mwenyewe si utukufu.

lakini matumbo yake, na miguu yake, ataosha kwa maji; na huyo kuhani atavisongeza vyote na kuviteketeza juu ya madhabahu; ni sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA.

Naye kuhani atavaa nguo yake ya kitani, na suruali zake za kitani atazivaa mwilini mwake; naye atayazoa majivu ambayo huo moto umeiteketezea sadaka juu ya madhabahu, kisha atayaweka kando ya madhabahu.

Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.

Akawaagiza, akasema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode.

Wakati huo, makutano walipokutanika maelfu, hata wakakanyagana, alianza kuwaambia wanafunzi wake kwanza, Jilindeni na chachu ya Mafarisayo, ambayo ni unafiki.

Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;

wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwahimiza wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.

Chachu kidogo huchachua donge zima.

Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo