Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 2:12 - Swahili Revised Union Version

12 Vitu hivyo mtavisongeza kwa BWANA kuwa ni malimbuko; lakini visifike juu ya madhabahu kuwa ni harufu ya kupendeza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Unaweza kumletea Mwenyezi-Mungu mazao yako ya kwanza kama sadaka. Lakini hayo hayatatolewa madhabahuni kama harufu ya kumpendeza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Unaweza kumletea Mwenyezi-Mungu mazao yako ya kwanza kama sadaka. Lakini hayo hayatatolewa madhabahuni kama harufu ya kumpendeza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Unaweza kumletea Mwenyezi-Mungu mazao yako ya kwanza kama sadaka. Lakini hayo hayatatolewa madhabahuni kama harufu ya kumpendeza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Unaweza kuzileta kwa Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya malimbuko, lakini haziwezi kutolewa juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kupendeza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Unaweza kuzileta kwa bwana kama sadaka ya malimbuko, lakini haziwezi kutolewa juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kupendeza.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Vitu hivyo mtavisongeza kwa BWANA kuwa ni malimbuko; lakini visifike juu ya madhabahu kuwa ni harufu ya kupendeza.

Tazama sura Nakili




Walawi 2:12
15 Marejeleo ya Msalaba  

Basi shamba la Efroni lililokuwa katika Makpela kuelekea Mamre, shamba, na pango lililokuwemo, na miti yote iliyokuwamo shambani, iliyokuwa katika mipaka yake pande zote, vyote viliyakinishwa


Mara amri ilipovavagaa, wana wa Israeli wakatoa kwa wingi malimbuko ya nafaka, divai, mafuta, asali, na mazao yote ya mashamba; na zaka za vitu vyote wakazileta kwa wingi.


Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako. Mzaliwa wa kwanza katika wanao wanaume utanipa mimi.


Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.


Nawe utaitunza sikukuu ya majuma, nayo ni ya malimbuko ya mavuno ya ngano, na sikukuu ya kukusanya vitu mwisho wa mwaka.


Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu;


Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa BWANA.


Ataleta matoleo yake, pamoja na mikate iliyotiwa chachu, na pamoja na sadaka zake za amani, kwa ajili ya shukrani.


Kutoka kwa unga wenu mtakaokanda kwanza wa chengachenga mtasongeza sadaka ya unga wa kuinuliwa uwe sadaka ya kuinuliwa; vile vile kama mfanyavyo sadaka ya kuinuliwa ya sakafu ya kupuchukulia nafaka, ndivyo mtakavyoiinua.


Yaliyo mazuri katika mafuta, na yaliyo mazuri ya mavuno ya zabibu, na ya mavuno ya nafaka, malimbuko yake watakayompa BWANA, hayo nimekupa wewe.


Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.


Na sasa, tazama, nimeleta malimbuko ya mazao ya ardhi uliyonipa, Ee BWANA. Kisha ukiweke chini mbele za BWANA, Mungu wako, ukasujudu mbele za BWANA, Mungu wako;


Hawa ndio wasiojitia unajisi na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo