Wana wa Israeli wakauona uso wa Musa ya kuwa ngozi ya uso wake Musa iling'aa; naye Musa akautia utaji juu ya uso wake tena, hata alipoingia kusema naye.
Mathayo 13:43 - Swahili Revised Union Version Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha, wale wema watangara kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio na asikie! Biblia Habari Njema - BHND Kisha, wale wema watangara kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio na asikie! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha, wale wema watang'ara kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio na asikie! Neno: Bibilia Takatifu Ndipo wenye haki watang’aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio, na asikie. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo wenye haki watang’aa kama jua katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu, Baba yao. Yeye aliye na masikio, na asikie. BIBLIA KISWAHILI Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie. |
Wana wa Israeli wakauona uso wa Musa ya kuwa ngozi ya uso wake Musa iling'aa; naye Musa akautia utaji juu ya uso wake tena, hata alipoingia kusema naye.
Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.
Kisha Mfalme atawaambia wale walioko katika mkono wake wa kulia, Njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
nilikuwa uchi, mkanivika nilikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nilikuwa kifungoni, mkanijia.
Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?