Matendo 2:13 - Swahili Revised Union Version Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini wengine wakawadhihaki wakisema, “Watu hawa wamelewa divai mpya!” Biblia Habari Njema - BHND Lakini wengine wakawadhihaki wakisema, “Watu hawa wamelewa divai mpya!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini wengine wakawadhihaki wakisema, “Watu hawa wamelewa divai mpya!” Neno: Bibilia Takatifu Lakini wengine wakawadhihaki wakasema, “Hawa wamelewa kwa divai!” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wengine wakawadhihaki wakasema, “Hawa wamelewa divai!” BIBLIA KISWAHILI Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya. |
Na kinywa chako kama divai iliyo bora, Kwa mpendwa wangu inashuka taratibu, Ikitiririka midomoni mwao walalao.
Na katika mlima huu BWANA wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.
Na watu wa Efraimu watakuwa kama shujaa, na moyo wao utafurahi kana kwamba ni kwa divai; naam, watoto wao wataona mambo haya, na kufurahi; mioyo yao itamfurahia BWANA.
BWANA wa majeshi atawalinda; Nao watakula na kuyakanyaga mawe ya teo; Nao watakunywa na kufanya kelele kama kwa divai; Nao watajazwa kama mabakuli, kama pembe za madhabahu.
Maana wema wake, jinsi ulivyo mwingi! Na uzuri wake, jinsi ulivyo mwingi! Nafaka itawasitawisha vijana wanaume, Na divai mpya vijana wanawake.
Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?