Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kulia, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.
Marko 9:27 - Swahili Revised Union Version Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Yesu akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama. Biblia Habari Njema - BHND Lakini Yesu akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Yesu akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Isa akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Isa akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama. BIBLIA KISWAHILI Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama. |
Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kulia, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.
Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka.
Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate katika macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?
Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa.
Alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
Yule jemadari akamshika mkono akajitenga pamoja naye kando, akamwuliza kwa faragha, Una neno gani utakalo kuniarifu?
Akamshika mkono wa kulia, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu.
Akampa mkono, akamwinua; hata kisha akawaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, akiwa hai.