Marko 15:5 - Swahili Revised Union Version Wala Yesu hakujibu neno tena, hata Pilato akastaajabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Yesu hakujibu neno, hata Pilato akashangaa. Biblia Habari Njema - BHND Lakini Yesu hakujibu neno, hata Pilato akashangaa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Yesu hakujibu neno, hata Pilato akashangaa. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Isa hakujibu lolote, hivyo Pilato akashangaa. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Isa hakujibu lolote, hivyo Pilato akashangaa. BIBLIA KISWAHILI Wala Yesu hakujibu neno tena, hata Pilato akastaajabu. |
Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.
Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa BWANA wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni.
Sikiliza sasa, Ee Yoshua, kuhani mkuu, wewe na wenzako wanaoketi mbele yako; maana hao ni watu walio ishara ya mambo yajayo; kwa maana, tazama, ninamleta mtumishi wangu, aitwaye Chipukizi.
Akaingia tena ndani ya ile Praitorio, akamwambia Yesu, Wewe umetoka wapi? Lakini Yesu hakumpa jibu lolote.
Maana nadhani ya kuwa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho, kama watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu.