Walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia,
Marko 14:26 - Swahili Revised Union Version Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda katika mlima wa Mizeituni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha wakaimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni. Biblia Habari Njema - BHND Kisha wakaimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha wakaimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni. Neno: Bibilia Takatifu Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni. Neno: Maandiko Matakatifu Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni. BIBLIA KISWAHILI Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda katika mlima wa Mizeituni. |
Walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia,
Amin, nawaambia ninyi, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu.
Akatoka akaenda mpaka mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa desturi yake; wanafunzi wake nao wakafuatana naye.
Alipokwisha kusema hayo, Yesu alitoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ng'ambo ya kijito Kedroni, palipokuwapo bustani; akaingia yeye na wanafunzi wake.
Lakini ilipokuwa karibu usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Kuna mtu miongoni mwenu anayeteseka? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.
Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,