Wakamwambia, Sisi watumwa wako tu ndugu kumi na wawili, wana wa mtu mmoja katika nchi ya Kanaani; na mdogo wetu yuko pamoja na baba yetu leo, na mmoja hayuko.
Maombolezo 5:7 - Swahili Revised Union Version Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wazee wetu walitenda dhambi na hawapo tena; nasi tunateseka kwa sababu ya makosa yao. Biblia Habari Njema - BHND Wazee wetu walitenda dhambi na hawapo tena; nasi tunateseka kwa sababu ya makosa yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wazee wetu walitenda dhambi na hawapo tena; nasi tunateseka kwa sababu ya makosa yao. Neno: Bibilia Takatifu Baba zetu walitenda dhambi na hawapo tena, na sisi tunachukua adhabu yao. Neno: Maandiko Matakatifu Baba zetu walitenda dhambi na hawapo tena, na sisi tunachukua adhabu yao. BIBLIA KISWAHILI Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao. |
Wakamwambia, Sisi watumwa wako tu ndugu kumi na wawili, wana wa mtu mmoja katika nchi ya Kanaani; na mdogo wetu yuko pamoja na baba yetu leo, na mmoja hayuko.
Yakobo baba yao akawaambia, Mmeniondolea watoto wangu; Yusufu hayuko, wala Simeoni hayuko, na Benyamini mnataka kumchukua naye; mambo hayo yote yamenipata mimi.
Nawe, je! Mbona hunisamehe makosa yangu, Na kuniondolea maovu yangu? Kwa kuwa sasa nitalala mavumbini; Nawe utanitafuta kwa bidii, lakini sitakuwapo.
Jicho lake huyo anionaye halitaniangalia tena; Macho yako yatanielekea, lakini sitakuwapo.
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Ndipo utakapowaambia, Ni kwa sababu baba zenu wameniacha mimi, asema BWANA, na kuwafuata miungu mingine, na kuwatumikia, na kuwaabudu, wakaniacha mimi, wasiishike torati yangu;
na ninyi mmetenda mabaya kupita baba zenu; maana angalieni, mnaenda kila mmoja wenu kwa ushupavu wa moyo wake mbaya, msinisikilize mimi;
BWANA asema hivi, Sauti imesikiwa Rama, kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake; asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako.
Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi.
Je! Maana yake ni nini hata mkatumia mithali hii katika Israeli, mkisema, Baba wamekula zabibu mbichi, nao watoto wakatiwa ganzi la meno?
BWANA ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa kwa njia yoyote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne.