Maombolezo 5:19 - Swahili Revised Union Version Wewe, BWANA, unadumu milele; Kiti chako cha enzi ni tangu kizazi hata kizazi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini wewe Mwenyezi-Mungu watawala milele, utawala wako wadumu vizazi vyote. Biblia Habari Njema - BHND Lakini wewe Mwenyezi-Mungu watawala milele, utawala wako wadumu vizazi vyote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini wewe Mwenyezi-Mungu watawala milele, utawala wako wadumu vizazi vyote. Neno: Bibilia Takatifu Wewe, Ee Mwenyezi Mungu unatawala milele, kiti chako cha enzi chadumu kizazi hadi kizazi. Neno: Maandiko Matakatifu Wewe, Ee bwana unatawala milele, kiti chako cha enzi chadumu kizazi hadi kizazi. BIBLIA KISWAHILI Wewe, BWANA, unadumu milele; Kiti chako cha enzi ni tangu kizazi hata kizazi. |
Ufalme wako ni ufalme wa milele, BWANA ni mwaminifu katika maneno yake yote, Na mwenye fadhili katika matendo yake yote Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele, Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.
Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye Juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
Ee BWANA, Mungu wangu, mtakatifu wangu, wewe si wa milele? Hatutakufa. Ee BWANA, umemwandikia hukumu, nawe, Ee Jabali, umemweka imara ili aadhibishwe.
Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi?
Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza.
Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.
Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.