Nilikuwa nimekasirika na watu wangu, niliutia unajisi urithi wangu, nikawatia mkononi mwako; wewe hukuwatendea rehema; kwa wazee uliifanya nira yako kuwa nzito sana.
Maombolezo 5:12 - Swahili Revised Union Version Wakuu hutundikwa kwa mikono yao; Nyuso za wazee hazipewi heshima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakuu wetu wametungikwa kwa mikono yao; wazee wetu hawapewi heshima yoyote. Biblia Habari Njema - BHND Wakuu wetu wametungikwa kwa mikono yao; wazee wetu hawapewi heshima yoyote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakuu wetu wametungikwa kwa mikono yao; wazee wetu hawapewi heshima yoyote. Neno: Bibilia Takatifu Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao, wazee hawapewi heshima. Neno: Maandiko Matakatifu Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao, wazee hawapewi heshima. BIBLIA KISWAHILI Wakuu hutundikwa kwa mikono yao; Nyuso za wazee hazipewi heshima. |
Nilikuwa nimekasirika na watu wangu, niliutia unajisi urithi wangu, nikawatia mkononi mwako; wewe hukuwatendea rehema; kwa wazee uliifanya nira yako kuwa nzito sana.
Wazee wa binti Sayuni huketi chini, Hunyamaza kimya; Wametupa mavumbi juu ya vichwa vyao, Wamejivika viunoni nguo za magunia; Wanawali wa Yerusalemu huinama vichwa vyao Kuielekea nchi.
Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?
Hasira ya BWANA imewatenga, Yeye hatawaangalia tena; Hawakujali nafsi za wale makuhani, Hawakuwaheshimu wazee wao.
Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi BWANA.