Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.
Maombolezo 3:50 - Swahili Revised Union Version Hata BWANA atakapoangalia Na kutazama toka mbinguni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema mpaka Mwenyezi-Mungu kutoka huko mbinguni aangalie chini na kuona. Biblia Habari Njema - BHND mpaka Mwenyezi-Mungu kutoka huko mbinguni aangalie chini na kuona. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza mpaka Mwenyezi-Mungu kutoka huko mbinguni aangalie chini na kuona. Neno: Bibilia Takatifu hadi Mwenyezi Mungu atazame chini kutoka mbinguni na kuona. Neno: Maandiko Matakatifu hadi bwana atazame chini kutoka mbinguni na kuona. BIBLIA KISWAHILI Hata BWANA atakapoangalia Na kutazama toka mbinguni. |
Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.
Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?
Jicho langu lanitia huzuni nafsini mwangu, Kwa ajili ya kuangamizwa kwa binti wa watu wangu.