Luka 8:7 - Swahili Revised Union Version Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyingine zilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti ya miiba ilipoota ikazisonga. Biblia Habari Njema - BHND Nyingine zilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti ya miiba ilipoota ikazisonga. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyingine zilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti ya miiba ilipoota ikazisonga. Neno: Bibilia Takatifu Nazo mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo ile miiba ikakua pamoja nazo, na kuisonga hiyo mimea. Neno: Maandiko Matakatifu Nazo mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo ile miiba ikakua pamoja nazo, na kuisonga hiyo mimea. BIBLIA KISWAHILI Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga. |
Maana BWANA awaambia hivi watu wa Yuda na Yerusalemu Ulimeni udongo katika konde zenu, wala msipande mbegu kati ya miiba.
Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;
Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lolote.
Nyingine zikaanguka penye udongo mzuri; zikamea, zikazaa moja kwa mia. Alipokuwa akinena hayo alipaza sauti akisema, Mwenye masikio ya kusikizia, na asikie.