Ametoa kwa ukarimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
Luka 6:30 - Swahili Revised Union Version Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyanganya mali yako usimtake akurudishie. Biblia Habari Njema - BHND Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyanganya mali yako usimtake akurudishie. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyang'anya mali yako usimtake akurudishie. Neno: Bibilia Takatifu Mpe kila akuombaye, na kama mtu akichukua mali yako usitake akurudishie. Neno: Maandiko Matakatifu Mpe kila akuombaye, na kama mtu akichukua mali yako usitake akurudishie. BIBLIA KISWAHILI Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie. |
Ametoa kwa ukarimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
Mimi nilipotia moyo wangu katika kuijua hekima, na kuuona utumishi uliofanyika juu ya nchi, (maana kuna asiyepata usingizi kwa macho yake mchana wala usiku);
Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.
Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili.
Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwizi, wala nondo haharibu.
Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate.
Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Katika mambo yote nimewaonesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
Mwizi asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akifanya kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.