Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 19:17 - Swahili Revised Union Version

17 Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Anayemsaidia maskini anamkopesha Mwenyezi-Mungu; Mwenyezi-Mungu atamlipa kwa tendo lake jema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Anayemsaidia maskini anamkopesha Mwenyezi-Mungu; Mwenyezi-Mungu atamlipa kwa tendo lake jema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Anayemsaidia maskini anamkopesha Mwenyezi-Mungu; Mwenyezi-Mungu atamlipa kwa tendo lake jema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Mwenyezi Mungu, naye atamtuza kwa aliyotenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Yeye amhurumiaye maskini humkopesha bwana, naye atamtuza kwa aliyotenda.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

17 Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.

Tazama sura Nakili




Methali 19:17
21 Marejeleo ya Msalaba  

naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma.


BWANA atamlinda na kumhifadhi hai, Naye atafanikiwa katika nchi; Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.


Atawahurumia wanyonge na maskini, Na nafsi za wahitaji ataziokoa.


Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake; Na atarudishiwa matendo ya mikono yake.


Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri.


Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu.


Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa; Maana huwapa maskini chakula chake.


Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.


Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.


Tupa chakula chako juu ya maji; Maana utakiona baada ya siku nyingi.


Uwagawie sehemu watu saba, hata wanane; Maana hujui baa gani litakalokuwa juu ya nchi.


Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.


Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.


Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili BWANA, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako.


Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.


Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo