Baa hilo ni katika mambo yote yanayofanyika chini ya jua, ya kuwa wote wanalo tukio moja; naam, zaidi ya hayo, mioyo ya wanadamu imejaa maovu, na wazimu umo mioyoni mwao wakati walipo hai, na baadaye huenda kwa wafu.
Luka 6:11 - Swahili Revised Union Version Wakajawa na uchungu, wakashauriana wao kwa wao wamtendeje Yesu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini wao wakakasirika sana, wakajadiliana jinsi ya kumtendea Yesu maovu. Biblia Habari Njema - BHND Lakini wao wakakasirika sana, wakajadiliana jinsi ya kumtendea Yesu maovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini wao wakakasirika sana, wakajadiliana jinsi ya kumtendea Yesu maovu. Neno: Bibilia Takatifu Wale wakuu wakakasirika sana, wakashauriana wao kwa wao ni nini watakachomtendea Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Wale wakuu wakakasirika sana, wakashauriana wao kwa wao ni nini watakachomtendea Isa. BIBLIA KISWAHILI Wakajawa na uchungu, wakashauriana wao kwa wao wamtendeje Yesu. |
Baa hilo ni katika mambo yote yanayofanyika chini ya jua, ya kuwa wote wanalo tukio moja; naam, zaidi ya hayo, mioyo ya wanadamu imejaa maovu, na wazimu umo mioyoni mwao wakati walipo hai, na baadaye huenda kwa wafu.
Wakuu wa makuhani na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao.
Akawakazia macho wote pande zote, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.
Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.
Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.
Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Yudea, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitaka kumwua.
Na mara nyingi katika masinagogi yote niliwaadhibu, nikawashurutisha kukufuru; nikawaonea hasira kama mwenye wazimu, nikawaudhi hata katika miji ya ugenini.
Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kama ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;
Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao wanaume wawili ulivyokuwa dhahiri.