Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.
Luka 5:16 - Swahili Revised Union Version Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini yeye alikwenda zake mahali pasipo na watu, akawa anasali huko. Biblia Habari Njema - BHND Lakini yeye alikwenda zake mahali pasipo na watu, akawa anasali huko. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini yeye alikwenda zake mahali pasipo na watu, akawa anasali huko. Neno: Bibilia Takatifu Lakini mara kwa mara Isa alijitenga nao ili kwenda mahali pa faragha kuomba. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini mara kwa mara Isa alijitenga nao ili kwenda mahali pa faragha kuomba. BIBLIA KISWAHILI Lakini yeye alikuwa akijitenga, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba. |
Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.
Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;
Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.
Baada ya maneno hayo yapata siku nane, aliwatwaa Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba.
Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta.
Kisha Yesu, alipotambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.