Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama waandishi.
Luka 4:32 - Swahili Revised Union Version wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakastaajabia uwezo aliokuwa nao katika kufundisha. Biblia Habari Njema - BHND Wakastaajabia uwezo aliokuwa nao katika kufundisha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakastaajabia uwezo aliokuwa nao katika kufundisha. Neno: Bibilia Takatifu Wakashangazwa sana na mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na mamlaka. Neno: Maandiko Matakatifu Wakashangazwa sana na mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na mamlaka. BIBLIA KISWAHILI wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo. |
Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama waandishi.
Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.
Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.
ya kwamba Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.