Luka 3:10 - Swahili Revised Union Version Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Umati wa watu ukamwuliza, “Tufanye nini basi?” Biblia Habari Njema - BHND Umati wa watu ukamwuliza, “Tufanye nini basi?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Umati wa watu ukamwuliza, “Tufanye nini basi?” Neno: Bibilia Takatifu Umati ule wa watu wakamuuliza, “Inatupasa tufanyeje basi?” Neno: Maandiko Matakatifu Ule umati wa watu ukamuuliza, “Inatupasa tufanyeje basi?” BIBLIA KISWAHILI Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi? |
Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtosheke na mishahara yenu.
Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Abrahamu watoto.
Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.