ukaniandalie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa.
Luka 24:50 - Swahili Revised Union Version Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha akawaongoza nje ya mji hadi Bethania, akainua mikono yake juu, akawabariki. Biblia Habari Njema - BHND Kisha akawaongoza nje ya mji hadi Bethania, akainua mikono yake juu, akawabariki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha akawaongoza nje ya mji hadi Bethania, akainua mikono yake juu, akawabariki. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya kuwaongoza hadi Bethania, akainua mikono yake juu na kuwabariki. Neno: Maandiko Matakatifu Akiisha kuwaongoza mpaka kwenye viunga vya Bethania, akainua mikono yake juu na kuwabariki. BIBLIA KISWAHILI Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki. |
ukaniandalie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa.
Yusufu akamwambia babaye, Hawa ni wanangu, Mungu alionipa nikiwa hapa. Akasema, Tafadhali uwalete kwangu nami nitawabariki.
Hayo yote ndiyo makabila ya Israeli kumi na mawili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa baraka zake aliwabariki.
Kisha Haruni akainua mikono yake na kuielekeza kwa hao watu, akawabariki; kisha akashuka akisha isongeza sadaka ya dhambi, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani.
Walipokaribia Yerusalemu karibu na Bethfage na Bethania, kukabili mlima wa Mizeituni, aliwatuma wawili katika wanafunzi wake,
Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato.
Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.
Basi, nataka wanaume waombe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.